SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) leo Machi 4, 2020, limesema utaratibu wa wachezaji kusalimiana kwa kushikana mikono kabla ya mechi hautatumika kuanzia leo kwenye mechi za Ligi Kuu na badala yake watasalimiana kwa ishara.
Uamuzi huo ni moja ya hatua za kujilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona. 