×

Mkunga Atenganisha Kichwa na Kiwiliwili cha Mtoto Mama Akijifungua

POLISI nchini Uganda, wanachunguza taarifa za mkunga ambaye anadaiwa kushindwa kumhudumia mjamzito na kusababisha mtoto kutengana kichwa na kiwiliwili wakati mama huyo akiwa anajifungua.

 

Gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti mkasa huo uliotokea mjini Busia likisema mama huyo alikuwa akijifungua na kichwa cha mtoto huyo kilitengana na kiwiliwili. Gazeti hilo limemnukuu mama huyo, Lilian Musazi, akidai kuwa muuguzi huyo alimvuta mtoto huyo miguu ambayo ndio ilianza kutoka.

 

Familia ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21 imesema mama huyo alipoingia kwenye chumba cha kujifungulia alisubiri sana kabla ya kuhudumiwa.

 

Lilian amekuwapo katika kituo cha afya cha Bulumbi nchini humo kwa siku nne akisubiri muda wa kujifungua ufike. Imeelezwa kuwa baadaye familia yake iliwasilisha ombi la kutaka kumhamisha mama huyo kwenda kwenye hospitali nyingine kama wangekuwa wametambua kuwa kuna tatizo.

Leave a Comment