×

NBC Kuendelea Kutoa Fursa za Ajira, Mafunzo Kwa Vijana

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobaid Sabi akizungumza katika mkutano wa mawaziri na wadau wa sekta ya kazi na ajira kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwaAfrika (SADC).
Makamu wa Rais wajamhuri ya muunganowa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akimpatia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobaid Sabi tuzo ya ushirikiano katika mpango mafunzo kwa Vijana unaoratibi wa Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA).

 

Mkugurenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Theobald Sabi amesema kuwa kwa mwaka huu wamejipanga kuchukua vijana zaidi ya 100 na kuwapatia ma-funzo ya uzoefu wa kazi yenye lengo la kuwatengeneza kuwa wanataaluma wa baadae pindi watakapoajiriwa kwenye sekta za kibenki nchini.

 

Aidha amesema hadi hivi sasa NBC imewapokea jumla ya vijana 146 ambao wame-wasambaza katika idara na vitengo mbali mbali ndani ya benki hiyo ambako wanafanya kazi zile zile zinazofanywa na watumishi wao walioajiriwa.

 

Sabi ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mawaziri na wadau wa utatu wa sekta ya kazi na ajira kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Ny-erere (JNICC).

 

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, NBC ilikuwa na jumla ya vijana 81 wanaopata mafunzo ya uzoefu wa kazi na Januari mwaka huu , iliongeza vijana 45 chini ya mpango huo huo na kufikisha jumla ya vijana 126 walioko katika benki hiyo hadi hivi sasa. Aidha NBC imewapa mikataba ya kudumu ya ajira vijana wanne ambao wamepangiwa kazi katika maeneo mbali mbali ya benki.

 

“Lengo letu ni kuongeza vijana 100 zaidi mwaka huu wa 2020 chini ya mpango wa mafunzo ya uzoefu wa Kazi. Kiukweli mpango wa Serikali wa mafunzo haya, ume-wawezesha NBC kuwapata vijana wa kitanzania, wenye taaluma tunazohitaji katika benki yetu, na wanafanyakazi katika idara mbali mbali,” alisema.

 

Hata hivyo alisema kwa mwaka 2018 walipokea vijana 44 na kati ya hao, vijana 39 walipatiwa mikataba ya miezi sita ambayo iliwaweze kujifunza, kupata uzoefu na ku-fanyakazi kwenye idara na vitengo mbali mbali ndani ya benki yao.

 

Alisema mpango huu wa mafunzo umefanikiwa kutokana na utaratibu mzuri unaorati-biwa na Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA) ya kuchuja vijana kutokana na misingi mitatu muhimu kama vile juhudi, nidhamu na uadilifu.

 

“Mpango huu wa mafunzo ya uzoefu wa Kazi ni mzuri, kwani unaondoa urasimu na gharama zisizokuwa za lazima katika kutafuta vijana kujaza nafasi zilizokuwa wazi.

Juhudi, Nidhamu, na Maadili ndizo nguzo kuu kwa vijana waliotayari kupata ajira ya kudumu kwenye sekta ya kibenki kupitia mpango huu wa mafunzo,” alisema.

 

“Hawa vijana tisa wenye mikataba ya mwaka mmoja pamoja na kuwalipa posho zao za kila mwezi, NBC inawapatia mafunzo ya stadi laini na stadi za kiufundi kama vile uongozi kwenye mauzo, huduma kwa wateja, mikopo, menejimenti ya mikopo chechefu, tija kwa makundi, na uwezeshaji wa mikopo kwa waagizaji na wauzaji bidhaa nje ya nchi,” alisema Sabi.

 

Awali Makamu wa Rais alifungua mkutano huo, Samia Sulubu Hassan alisema ukosefu wa ajira kwa vijana umebaki kuwa changamoto ya kidunia na kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kuhusu mwenendo wa soko la ajira kwa mwaka huu inaonesha zaidi ya watu Milioni 187.7 duniani hawana kazi.

Amesema, katika kuelekea siku ya wanawake duniani sekta ya kazi na ajira kuna mambo mengi ya kuangalia ili kuweza kupunguza udhalulishaji wa wanawake makazini pamoja na kuangalia usawa wa kijinsia katika sehemu za kazi.

 

Amewaomba viongozi kufanya maamuzi, kuyatakekeleza na kusimamia yale yote yanayoazimiwa na kutolewa maamuzi kwa kushirikiana na wadau wa utatu.

 

Alisema kwa katika Jumuiya ya SSDC inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya nguvu kazi ni vijana hivyo hawana budi kuitumia ipasvyo katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini.

 

Kuhusu National Bank of Commerce (NBC)

Benki ya Taifa ya Biashara, NBC ni benki ya zamani kuliko zote nchini Tanzania ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitano. Tunatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wa rejareja, biashara, mashirika na misaada ya uwekezaji, bidhaa na huduma za usi-mamizi mzuri wa fedha.

 

Benki hii inaanzia mwaka 1967 ambapo Serikali ya Tanzania ilibinafsisha taasisi zote za fedha, zikiwamo benki. Mwaka 1991, sheria ya mabenki ilirekebishwa na miaka sita baadae, yaan mwaka 1997, taasisi iliyojulikana kama Benki ya Taifa ya biashara, ili-gawanywa ka;ka tanzu tatu tofau;: NBC Holding Corpora;on, Na;onal Microfiance Bank (NMB) na NBC (1997) Limited. Mwaka 2000, Benki ya Afrika Kusini, Absa Group Limited, ilipata hisa 55% kutoka NBC (1997) Limited. Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tan-zania ilipata 30% ya hisa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) kama mwanachama wa Benki ya dunia (World Bank Group), ilipata 15% ya hisa za benki hii. Taasisi hiyo mpya ikaitwa NBC Limited.

 

Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopa;kana ka;ka maeneo mbalimbali nchini. Ikiwa na matawi 5 na mashine za ATM zaidi ya 230, Benki ya NBC inatoa hudu-ma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbal-imbali. Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,200 nchi nzima.

 

Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us [email protected]

Leave a Comment