PROMOSHENI kubwa ya kihistoria inayotikisa kwa sasa nchini, yaani Bahati Nasibu ya Shinda Gari inayoendeshwa na magazeti ya Championi na Spoti Xtra yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers imezidi kuchanja mbuga na leo imetia timu katika maeneo ya Chamazi, Mbagala Rangi Tatu na Majimatitu jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa maeneo hayo, wamejitokeza kwa wingi kununua Gazeti la Championi ambalo lipo mtaani leo Jumamosi na kujaza kuponi za kushiriki bahati nasibu hiyo huku wengi wao wakionyesha kiu ya kushinda Ndinga Mpya hiyo aina ya Toyota FunCargo itakayotolewa kwa mshindi wa droo kubwa itakayochezeshwa miezi mitatu ijayo.
Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo wakati wa promosheni hiyo, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Antony Adam, amesema ili kuingia kwenye droo kubwa ya kushinda gari, wasomaji wanatakiwa kununua magazeti ya Championi (Tsh 800) na Spoti Extra (Tsh 500), na kujaza kuponi iliyopo kwenye ukurasa wa pili wa magazeti hayo kisha kufuata masharti yaliyoainishwa hapo.
“Msomaji yeyote anaweza kujishindia zawadi hiyo kubwa ya Ndinga Mpya ya FunCargo na zawadi nyingine kama simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio,” alisema Anthony.
JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.
MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.









