LIONEL Messi na Cristiano Ronaldo hawatakuwa uwanjani milele, wote wamekaribia kufikia mwisho wa enzi zao, lakini gwiji Dimitar Berbatov amesema mrithi wa nyota hao, ni Mnorway, Erling Haaland.
Nyota mwenye miaka 21 wa PSG, Kylian Mbappé, naye ameonekana kuwa m p a m banaji anayeweza kuchukua sifa za Messi na Ronaldo akiwa ameshafunga mabao 30 msimu huu. Lakini Haaland, ndiye amekuwa gumzo zaidi akiendelea kutamba nchini Ujerumani katika kikosi cha Borussia Dortmund.
Mnorway huyo, 19, alijitambulisha kwenye ulimwengu wa soka kwa kufunga hat trick kwenye mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa akiichezea RB Salzburg, Septemba. Miezi minne baadaye, alifunga hat trick nyingine akiichezea Dortmund mechi yake ya kwanza, baada ya hapo alifunga mabao mengine saba kwenye michuano yote akiichezea miamba hiyo ya Bundesliga, yakiwemo m a b a o mawili dhidi ya PSG ya Mbappe.
Tayari Haaland ana mabao 40 msimu huu akizichezea Salzburg na Dortmund, na inaaminika kuna mengi yanafuata. Hata Messi mwenyewe alifunga mabao 16 tu katika msimu wake mzima Barcelona 2007-08, wakati Ronaldo alifunga mabao sita katika msimu wake wa kwanza Man United.
“Ni mchezaji mwenye kipaji cha ajabu na kwangu mimi kuna uwezekano akawa mrithi wa Messi na Ronaldo, siyo yeye pekee, lakini nampenda Mbappe pia, anawachezea mabeki atakavyo,” alisema Berbatov.
“Tunahitaji kuvuta subira tukitarajia wachezaji hawa watabaki na afya na kuendelea kujiboresha ili tuwaone kwa muda mrefu.”
MUNICH, Ujerumani
