KOCHA Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema mastraika wake Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah wamekuwa wakimuumiza kichwa kila anapokuwa anapanga kikosi cha kuanza mchezo husika.
Arteta alisema hayo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya West Ham juzi na kubakiza pointi tano kabla ya kuifi kia Chelsea kwenye top 4 Premier, bao hilo pekee likifungwa na Lacazette. Nketiah aliuanza mchezo huo lakini alimpisha Lacazette dakika ya 59 ambaye alikwenda kufunga.
Arteta anaamini wote, Lacazette, 28, na Nketiah, 20, wapo kwenye kiwango bora kwa sasa na wanampa wakati mgumu wa kuchagua nani aanze.
“Nina mastraika wawili kwa sasa ambao wananipa ugumu lakini ni jambo zuri. Wote wanafunga, wote wapo kwenye hali nzuri,” alisema Arteta.
