×

Amuua Kaka Yake; Alimkuta Kitandani na Mama Yao

MWANAMME mmoja (35)   ambaye hakutajwa jina, mkazi wa kijiji cha Chegati, Kaunti ya Kisii, Kenya, ameuawa kwa kukatwa mapanga na mdogo wake kwa madai kwamba alikuwa akifanya mapenzi na mama yao mzazi.

Majirani walisema kwamba marehemu alikuwa akifanya mapenzi na mama (55) yake kwa muda mrefu na kwamba jambo hilo lilikuwa linajulikana.

Mdogo mtu huyo baada ya kuvunja dirisha na kuingia ndani aliwafuma wawili hao wakiwa kitandani huku wamelewa na ndipo akamshambulia kaka yake kwa panga.

Inadaiwa alilazimika kuvunja dirisha kwani alipogonga mlango marehemu na mama yake hawakufungua, licha ya kuwasikia wakiongea ndani.

Dada wa marehemu alinukuliwa akisema kaka yake huyo alikuwa hajaoa na alikuwa akikaa nyumbani kwa mama yake muda mrefu usiku kila siku kabla ya kuondoka.

Baba wa familia hiyo hufanya kazi mjini Nairobi na hajaonekana nyumbani kwa muda wa miezi miwili iliyopita.

Mama huyo amekamatwa, na anayedaiwa kuua bado anasakwa.

Leave a Comment