×

Marekani Yaongoza Kuuza Silaha Duniani

RIPOTI mpya imeonyesha kwamba Marekani imeongoza kwa kuuza silaha za kivita kuliko nchi nyingine yoyote duniani huku silaha nyingi zikipelekwa Mashariki ya Kati kwenye migogoro mingi.

 

Ripoti iliyotolewa na taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani  ya Stockhlom, Sweden,  (SIPRI) imeonyesha pia mpaka sasa hakuna nchi iliyonunua silaha nyingi zaidi kuliko Saudi Arabia.

 

Pia imeonysha kwamba biashara ya kimataifa ya silaha imepanda kwa zaidi ya asilimia tano kuanzia mwaka 2015-2019 ambapo tangu mwaka 2015 asilimia 61 ya silaha zimeuzwa Mashariki ya Kati.

Leave a Comment