×

Halima Mdee Amwaga Machozi Akitoka Gerezani

MBUNGE Halima Mdee amemwaga machozi hadharani baada ya kutoka gereza la Segerea leo na kuwashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha wa kuwachangia na kuwafanyaa wao kuwa nje ya gereza.

Watanzania nyie hamjui, hamjui mlivyotusitiri mimi ni kamanda lakini napata hisia, nilikua najua tulivyonyong’onyezwa ila watu wametuchangia tunashukuru na bado pesa zinaingia. Mimi nalia sio kwamba naogopa hapana ila upendo wenu muliouonyesha kwetu.

“Nawashukuru sana Watanzania, walijua hatuna fedha, ni kweli hatukuwa na pesa kabisa, walijua mapema tunaenda jela. Walishafunga akaunti zote hadi za mwenyekiti wetu Mbowe, wakaangalia sisi wengine hali zetu tusingeweza kulipa fidia hizo,” alisema Mdee huku akilia.

 

Wabunge Halima Mdee, Esther Matiko na Ester Bulaya wametoka gereza la Segerea leo baada ya kulipa faini ya Sh110 milioni.

 

Leave a Comment