×

Magufuli Alipa Mil. 38 Kumtoa Msigwa Jela

RAIS John Magufuli leo Machi 12, 2020,  amemlipia Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa Sh. milioni 38  milioni 40 alizotakiwa kulipa ili atoke jela kutokana na hukumu iliyopitishwa wiki hii na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa, amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya ndugu kuchanga na kupata milioni mbili tu na hivyo kumtafuta Magufuli ili kupata msaada.

 

“Sisi kama familia, tulikwenda kwa ndugu yetu Magufuli, tukamueleza tumekusanya Sh. 2 milioni na kwamba tunaomba naye achangie. Mheshimiwa Magufuli, akatoa mchango huo mara moja,” ameeleza ndugu mmoja wa Msigwa ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

 

Mbunge huyo wa Iringa Mjini, ni miongoni mwa washtakiwa wanane ambao ni viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliotiwa hatiani juzi Jumanne na mahakama hiyo ya Kisutu.

Leave a Comment