ILE PROMOSHENI kubwa nchini ya Bahati Nasibu ambayo mshindi wa droo kubwa anatarajia kujishindia ndinga mpya kwa kusoma magazeti ya Championi na Spoti Xtra, leo Jumatatu, Machi 16, 2020, imetikisa maeneo ya Kibaha Pwani na vitongoji vyake.
Kikosi cha idara ya mauzo na usambazaji cha magazeti bora ya michezo nchini, Championi na Spoti Xtra yanayochapishwa na Global Publishers kimetia timu maeneo hayo na kuwatangazia neema hiyo wasomaji wa magazeti hayo yanayoongoza kwa ubora wa habari za michezo na burudani.
Sambamba na Kibaha kikosi hicho kilipitia na kuzungumza na wasomaji wa Kiluvya, Maramba Mawili, Kinyerezi, Seregerea na Buguruni.
Akizungumza na wasomaji Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Global Publishers, Anthony Adam amewaeleza wasomaji hao wanunue magazeti hayo na kuijaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili kisha kumkabidhi yeye na kikosi chake au muuza magazeti yeyote aliye karibu naye.
Anthony amesema wasomaji hao sambamba na kujishindia gari aina ya Fun Cargo kuna zawadi zingine mbalimbali kama vile simu za mkononi maarufu kwa jina la Smart Kitochi na nyinginezo ambazo zitakuwa zikitolewa kila mwezi kuelekea kwenye droo kubwa ambayo mshindi ataibuka na ndinga hiyo mpya.
JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi au Spoti Xtra kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam. Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.
MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda.
Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.
HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS/GPL












