MSANII wa Bongo Fleva, Haitham Kim, amewaacha mashabiki vinywa wazi baada ya kutangaza kuwa anapania kuolewa na wanaume watatu ambao watakuwa na jukumu la kumlinda, kumrishisha wakati wa mapenzi na kutoa mahitaji yote ambayo mwanamke anastahili kupewa.
Akielezea ni kwa nini ameamua kuchukua hatua hiyo, Haitham aliongeza kuwa hataki kuumizwa na mwanamme mmoja wakati ambapo wengine wako wanaomtamani.
“Inawezekana nikaolewa na wanaume watatu kama watanimudu vizuri, unajua wanawake tunapenda wanaume watuonyeshe upendo, mahaba na kunijali kwa hiyo wakitokea wa kufanya yote hayo nipo tayari, pia siwezi kuumia kwa mtu mmoja wakati kuna wengine wananihitaji kwa muda huo,” alisema Haitham.
Mila na tamaduni za Kiafrika kwa wingi huwa haziruhusu mwanamke kuolewa na zaidi ya mwanamme mmoja, suala ambalo amelitupilia mbali akisema ana uwezo wa kuhimili wanaume hao.
“Mimi sina shida katika kuolewa na wanaume watatu, nina uwezo wa kuwashughulikia ipasavyo, iwe ni kitandani ama popote pale, nafahamu kuwa nina kisima kikubwa cha asali ambacho wote nina imani kuwa watatosheka,” alisema Haitham.
