×

Mtoto Baraka Atunukiwa Tuzo na Madaktari Muhimbili – Video

KWA mara nyingine tena, mtoto Baraka Shigongo mwenye ufahamu wa hali ya juu wa masuala mbalimbali ya Sayansi ya Afya ya Binadamu, ameendelea kuonesha Ulimwengu kipaji chake kwa kufundisha mambo mbalimbali makubwa yanayohusu afya ya miili yetu.

 

Baada ya kutua katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shiriki Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam na kuwafundisha wanafunzi wa fani ya udaktari, maabara, famasia na uhudumu afya chuoni hapo, mtoto huyo amebahatika kutunukiwa tuzo ya kutambua kipaji chake hicho ambacho kimekuwa kikiwavutia wengi.

 

Baraka (9) alivunja topic nne ikiwa ni Neurone, Nephron, Nervous System, Skeletal System ndani ya dakika 30 na kuwaacha midomo wazi madaktari hayo ambao waliamua kumtunuku tuzo hiyo ili kumpa moyo na kuwahamasisha watoto wengine kuiga anachokifanya Baraka.

Tazama Baraka anavyokudadavulia hapa

Leave a Comment