




Adam (kushoto) akimpatia zawadi ya sabuni mmoja wa wasomaji wa magazeti ya championi baada ya kukata kuponi yake. Hiyo inatokana na kuunga juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wananawa mikono kwa kutumia sabuni kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona.


ZIKIWA zimebaki siku chache kuchezeshwa kwa droo ndogo ya bahati nasibu ya Shinda Gari Mpya. Bahati Nasibu hiyo iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya inapatikana kupitia magazeti ya Championi na Spoti Xtra ambapo wasomaji wa magazeti hayo wa maeneo ya Mji Mwema, Vijibweni, Tungi na maeneo ya Feri Kigamboni jijini Dar es Salaam wameahidi kusepa kuelekea ndinga hiyo kutokana wanavyochangamkia magazeti hayo kwa kuyanunua na kukata kuponi.
Mapema leo timu ya maofisa masoko wa Global Publishers walitembelea maeneo hayo na kushuhudia umati wa watu wakijaza kuponi na kwa ajili ya kuingia katika droo ya bahati nasibu hiyo ambayo mshindi atanyakua ndinga mpya aina ya FunCargo..
Akipiga stori na wasomaji hao Ofisa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam, amewasisitiza wananchi hao kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili waweze kuwa miongoni mwa washindi wataoinyakua ndinga hiyo.
‘Niwasihi wakazi wa Kigamboni mwendelee kununua magazeti yetu ili muwe miongoni mwa washindi, tutatoa gari mpya siku ya mwisho ya droo na kabla ya droo kubwa wapo ambao kila wiki watakuwa wanajinyakulia simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.
JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.
MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.