×

Kura 14 Za Ndio Zamwondoa Meya Iringa Madarakani

Wajumbe wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa nchini Tanzania Jumamosi Machi 28, 2020 wamemuondoa madarakani meya wa manispaa hiyo, Alex Kimbe.

 

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa, mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Ryata amesema wajumbe waliohudhuria kikao ni 26 na kura 14 zimeridhia kumuondoa meya huyo.

 

“Ndugu zangu wajumbe, kura zilizopigwa ni 26, kura zilizoharibika ni 12, kura halali ni 14 na kura za ndio ni 14 na hapana ni kura zero (sifuri), hivyo Baraza la leo limepiga kura kihalali na taratibu zote zimezingatiwa,” alisema Ryata

“Kuanzia lMachi 28, 2020 Alex Kimbe hatakuwa meya hadi taratibu zitakavyofuata na baada ya kusema hayo naomba mkurugenzi uahirishe kikao” amesema

Leave a Comment