×

Madaktari Waomba Vifaa Kujikinga na Corona – Video


CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT) kimeiomba serikali kuhakikisha inawapa madaktari na wauguzi vifaa vya kujikinga na ugonjwa unaotokana na wa virusi vya corona (Covid-19) ili wasipate maambukizi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 2, 2020, Rais wa MAT, Dkt.  Elisha Osati, amesema vifaa vya kujikinga ni muhimu kwao ikizingatiwa idadi ya wagonjwa na walio katika hatari ya kupata maambukizi inaongezeka siku hadi siku.

 

“Tunadhani kuna nguvu inatakiwa kuongezwa hivyo tahadhari ni muhimu sana kwa sababu dunia nzima wanalia na uhaba wa vifaa,” amesema.

 

Ameishauri serikali kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye kliniki za magonjwa mengine kama kisukari na ukimwi kwa kutoa dawa za muda mrefu.

 

“Mfano wagonjwa wale wa kisukari, shinikizo la damu, maumivu ya migongo na misuli wanaweza kupewa dawa walau za miezi mitatu kwa sababu hawa wana uwezekano wa kupata ugonjwa mkali zaidi,” amesema.

Leave a Comment