×

Morrison: Luis Anatisha, Amekamilika Vilivyo

KIUNGO mshambuliaji hatari wa Yanga, Bernard Morrison amefunguka kuwa staa wa Simba, Luis Jose Miquissone ni mchezaji aliyekamilika na anatisha kwa wapinzani wote ambao anakutana nao.

 

Morrison amesema Miquissone ni mchezaji ambaye anamkubali kutokana na kujiamini sambamba na kuwa na tekiniki nyingi anapokuwa na mpira.

 

Morrison na Miquissone wote kwa pamoja walisajiliwa na timu zao katika dirisha dogo la usajili ambapo wote wamezifungia timu zao mabao matatu.

 

Morrison ameliambia Spoti Xtra, kuwa anamkubali Miquissone kwa sababu ni mchezaji ambaye ameka-milika akiwa hatari kwa wapinzani ambao anakutana nao huku akiwa na uwezo mkubwa anapokuwa na mpira.

 

“Luis ni mchezaji mzuri na binafsi ninamkubali sana, kwa sababu anajiamini na ana tekiniki nzuri anapokuwa na mpira.

 

“Ni mtu hatari kwa wapinzani anaocheza nao kwenye mechi za ligi. Lakini ni mchezaji ambaye amekamilika, lakini kuhusiana na kuendelea kubakia Simba kwa kwa muda mrefu ni suala la yeye mwenyewe kuamua kwani ndiye ambaye atapanga juu ya maisha yake ya mbele,” alisema Morrison.

STORI NA SAID ALLY NA MUSA MATEJA, CHAMPIONI

Leave a Comment