×

Chui Akutwa na Virusi vya Corona

CHUIMILIA wa miaka minne katika bustani ya wanyamapori (zoo) jijini New York amethibitishwa kuwa na maambukizi ya #Coronavirus yanayosababisha ugonjwa unaojulikana kama Covid-19.

 

Chui huyo ambaye anafahamika kwa jina la Nadia anaaminika kuwa mnyama kwa kwanza kuambukizwa ugonjwa huo kutoka kwa binadamu.

Maambukizi hayo yamethibitishwa na Maabara ya Taifa ya Huduma za Wanyama, na imeelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Nadia na wanyama wengine sita wameambukizwa na mhudumu.

 

Daktari Mkuu katika bustani hiyo, Paul Calle, amesema kwa ufahamu wao, hii inakuwa mara ya kwanza kwa mnyama kuumwa baada ya kupata maambukizi kutoka kwa binadamu.

Aidha, taarifa iliyotolewa na bustani hiyo imesema wanyama hao wote wapo chini ya uangalizi na inatarajiwa kuwa watapona.

 

Leave a Comment