×

Azam FC Kushusha Wachezaji Wanne Matata

UONGOZI wa Azam FC umeamua kuweka wazi dhamira yao ya kutaka kushindana na klabu kongwe katika Ligi Kuu Bara, Simba na Yanga katika masuala ya usajili wa wachezaji watakaokiimarisha kikosi chao kwa ajili ya kupindua utawala wa timu hizo.

 

Awali. Azam FC waliweza kupindua utawala wa timu hizo msimu wa 2013/2014 baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu ilipopanda kwa kufikisha pointi 59 ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ambazo zilikuwa haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

 

Taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata ni kwamba, uongozi wa timu hiyo umepanga kuwapiga chini baadhi ya nyota wake mwishoni mwa msimu huu baada ya kushindwa kuonyesha viwango bora huku wakipania kuwanasa nyota wengine kutoka nje.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakaria Thabit, ambaye alisema ni kweli wana mpango wa kufanya usajili wa wachezaji wengine kutoka nje kwa ajili ya kuongeza changamoto na ushindani na ndani kikosi hicho ambacho kina malengo ya kuangusha utawala wa Simba na Yanga.

 

“Ni kweli tuna mipango ya kufanya usajili, kwa sababu sisi ni timu kubwa na sifa ya timu kubwa yoyote duniani ni lazima ifanye usajili, kwa hiyo hata sisi tunataka kusajili wachezaji wengine wanne kutoka nje ili tuboreshe kikosi chetu, tunataka kipa, beki, kiungo na mshambuliaji.

 

“Hatufanyi hivi kwa kuwa tuna pengo sehemu yoyote ila ni kwa ajili ya kuwatengenezea changamoto na bidii wachezaji wetu,” alisema Zakaria.

Stori: Na Abdulghafal Ally

SPOTI HAUSI: USAJILI wa MAKAMBO YANGA / Huku OKWI Kurudi SIMBA / SURE BOY YANGA…

Leave a Comment