MAAMBUKIZI ya Virusi vya Corona duniani yanazidi kushika kasi. Hadi sasa nchi 209 duniani zimeathirika na virusi hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 74,795 hadi kufi kia April 7 mwaka huu.
Watu milioni 1.3 duniani tayari wameambukizwa virusi hivyo, hata zile nchi chache zilizonusurika kupatwa na virusi hivyo, tayari zimeanza kuripoti visa hivyo.
Virusi hivyo vilivyoanza kusambaa barani Asia katika nchi ya China, vimeathiri zaidi bara la Ulaya ambapo nchi za Uingereza, Italia na Ufaransa zilionekana kuelemewa na maambukizi pamoja na vifo vitokanavyo na Corona.
Jambo la kushangaza, madaktari wawili wa nchini Ufaransa waliona majaribio ya chanjo za virusi hivyo yanafaa kufanyiwa watu weusi, yaani Waafrika.
Hili ni jambo lililoamsha hasira za Waafrika wengi ikiwamo Wazungu kwa kuwa mara nyingi dawa za majaribio hufanywa kwa wanyama kama vile nyani na panya. Kwa mantiki hiyo, dhana ya madaktari hao ilikuwa sawa na tusi kwa Waafrika.
Dk. Jean-paul Mira, ambaye ni mkuu wa kitengo cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Cochin mjini Paris nchini Ufaransa, na Dk. Camille Locht, ambaye ni Mkuu wa utafi ti wa afya kutoka katika kikundi cha Inserm, wote walikaririwa na televisheni ya Ufaransa wakisema kuwa kuna kesi ya kufanya majaribio katika nchi za Afrika.
Wote wawili wameshambuliwa vikali kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakisema kauli yao hiyo ilikuwa ni ya ubaguzi wa rangi.
Kutokana na wengi kuonekana kuwashambulia, Inserm walilazimika kujitokeza na kufafanua kwamba, madaktari hao hawakueleweka vizuri.
WALICHOSEMA MADAKTARI HAO
Wakizungumza katika kituo cha LCI cha televisheni, madaktari hao walisema “Kama naweza kuchochea, je! Hatupaswi kufanya utafi ti huu barani Afrika, ambako hakuna mask, hakuna matibabu, hakuna kupona?” Dk. Mira.
“Kidogo kama ilivyofanyika mahali kwingine katika baadhi ya tafi ti kuhusu Ukimwi. Kwa mfano kwa makahaba, kwa sababu tunajaribu vitu kwa kuwa tunajua wamejianika na hawajilindi… uko sahihi”,” Dk. Locht alijibu.
“Tuko katika mchakato wa kufi kiria juu ya utafi ti kwa kutizama bara la Afrika,” alisema.
MSAMAHA
Kulingana na US News, Mira aliwaomba radhi wale ambao walikerwa na matamshi yake na hata kuhisi kudhalilishwa na kuropokwa kwake wakati wa mahojiano na runinga moja siku ya Jumatano, Aprili 1.
“Ningependa kuomba msamaha wale ambao nimewakosea, nimewashtua na kuhisi kutukanwa na matamshi yangu niliyoyatoa kwenye LCI wiki hii,” alisema daktari huyo.
WALIVYOSHAMBULIWA
Kauli hizo zilipokelewa kwa hasira kwenye mitandao ya kijamii na hata Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani naye alioneshwa kukasirishwa na kauli za madaktari hao. Mkurugenzi huyo, Dk. Tedros ambaye ni raia wa Ethiopia, alisema Afrika haiwezi na wala haitokua uwanja wa majaribio kwa chanjo yoyote.
“Imekasirishwa na kusikitishwa kuona karne hii kuna Wanasayansi wanatoa maoni kama hayo ya kibaguzi, tunawahakikishia hilo halitotokea” alisema.
Wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani Didier Drogba na Samuel Eto’o ni miongoni mwa watu waliokasirishwa na kauli za madaktari hao. “Ningependa kukemea waziwazi hizo dharau, uwongo na zaidi ya maneno yote ya ubaguzi,” aliandika Drogba kupitia akaunti yake ya Tweeter.
“Usichukulie watu wa Afrika kama nguruwe, inaumiza sana,” aliongeza. Kwa upande wake Eto’o aliwaita madaktari hao ‘wauaji’. Lakini Inserm katika taarifa yao walisema kuwa kauli za madaktari hao zilitafsiriwa tofauti”.
“Majaribio ya kliniki ya kujaribu ufanisi wa chanjo ya BCG dhidi ya Covid-19 (virusi vya corona) yataanza kuzinduliwa katika nchi za Ulaya na Australia.” Ilisema taarifa hiyo na kuongeza;
“Ikiwa kweli tunataka kupata taswira ipelekwe Afrika, ingefanyika sambamba na hizi. Afrika haifai kusahaulika au kutengwa na utafi ti kwa sababu janga ni la ulimwengu,” ilieleza taarifa hiyo.
Seneta wa Bungoma nchini Kenya, Moses Wetang’ula pia alimsuta daktari huyo. Katika ujumbe wenye maneno makali, kiongozi huyo wa chama cha FORD Kenya aliwataka viongozi wa Afrika kukataa jaribio hilo la kuwatumia Waafrika kama ‘nguruwe wa Guinea’.
“Chimbuko la COVID-19 (virusi vya Corona) ni China, Italy, Spain, Ufaransa na Marekani. Jaribio la tiba yake lazima ianze kule wala sio taifa lolote la Afrika,” “Viongozi wa Afrika lazima wakapinge jaribio lolote kwa watu wao kama nguruwe wa Guinea,” aliandika Wetangula.
CHANJO HII HAPA
BCG ni chanjo inayotolewa kwa watoto katika nchi ambazo zina maambukizi makubwa ya kifua kikuu.
Baadhi ya tafi ti zilizofanyika hivi karibuni zinapendekeza kuwa katika nchi ambazo chanjo ya BCG imetekelezwa vizuri, kuna vifo vichache vilivyotokana na virusi vya corona.
Hadi sasa, Afrika ni bara pekee ambalo lina maambukizi machache ya virusi vya Corona, ingawa visa vinavyothibitishwa na vifo vinaongezeka.
Hadi kufi kia Aprili 7 mwaka huu, nchi 52 zilikuwa zimeripoti visa 9,867 vya maambukizi ya Corona, vifo 482 huku watu 947 wakiripotiwa kupona virusi hivyo.
MAKALA NA MITANDAO
