×

Manara: Bao la Morrison Niliangalia WhatsApp

MSEMAJI Mkuu wa Simba, Haji Manara amefunguka kuwa bao ambalo walifungwa na Yanga kwenye mechi ya Dabi ya Kariakoo Machi 8, aliliangalia kwenye Makundi ya WhatsApp baada ya kushindwa kutazama mechi hiyo.

 

Manara amesema kwamba bao hilo halishindwa kulitazama kwa sababu alizima simu zake ambazo zilikuwa na uwezo wa kutazama mechi hiyo. Wakati wa mechi hiyo Manara alikuwa nchini Hispania.

 

Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison na kuifanya Yanga kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Akizungumza na Global TV katika mahojiano maalum, Manara alisema kwamba mechi nzima kati ya timu hizo aliifuatilia kwa kupitia komenti za makundi ya WhatsApp baada ya kuzima simu ambayo alikuwa akiiangalia mechi hiyo mwanzoni tu mwa mechi.

“Sikuwepo bahati mbaya, mechi ilinikuta nikiwa Hispania na usiku kulikuwa na mechi ya Madrid, nikawaomba ruhusa wenyeji wetu kuwa leo sitafanya vitu vyao nikasema niwaombe niangalie mechi.

 

“Mpira ulivyoanza nikazima simu, sikutaka kuangalia nikawa nasoma mechi kupitia komenti za WhatsApp, ndiyo zikawa zinanipa muelekeo wa mchezo, nikawa najua matokeo hadi tunafungwa bao.

 

“Ilipofika dakika 20 kabla ya mechi kuisha presha sasa ikawa imepanda, nikawa natembea kwenye korido kama dakika 20 au 25, kamera za CCTV zikanidaka.

 

“Nilikuwa natembea nikijua kwamba nikija kushika simu tunaweza tukawa tumerudisha, nilikuwa najiamini kwamba tutarudisha tu, sasa watu wa CCTV wakapata mshangao wakaja kuniuliza huyu ana nini, wakawa wanajiuliza huyu kapata kichaa, sikutaka kuwajibu kwa maneno nikaingia chumbani nikawaonyesha kwenye simu kwamba hapa tumeshafungwa.

 

“Wakacheka sana wakanipa pole, kabla ya dakika mbili kuisha Diamond akanipigia simu nikamwambia aache kila kitu nikasikia simu yake ameiangusha baadaye akaniuliza kwamba tushafungwa, sikuona ile mechi ila baadaye niliporudi nikaiangalia mechi na Yanga walistahili kushinda kwa sababu wachezaji wao walikuwa wanangongana na wanajitoa,” alisema Manara.

Mwandishi Wetu

Leave a Comment