×

Lwakatare Aaga Rasmi Bungeni: “Sigombei Tena” – Video

MBUNGE wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (Chadema) ameaga rasmi bungeni kuwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu 20202 hatagombea ubunge badala yake anawatakia mafanikio na kuwaachia nafasi hiyo watu wengine.

 

Lwakatare ametoa kauli hiyo leo Jumannne, Aprili 14, 2020 ndani ya bunge wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) ambapo ametaja mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake akijivunia kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania.

 

Mbunge huyo anakuwa wa pili kuaga kuwa hatagombea katika mkutano huu unaoendelea jijini Dodoma akitanguliwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) ambaye tayari alishaaga na kusema hagombei tena, hivyo kufanya majimbo mawili ya Mkoa wa Kagera kuwa yatakuwa na wabunge wapya.

Leave a Comment