MBUNGE wa Iramba (CCM), Dkt. Mwigulu Nchemba ameishauri serikali kuacha kutangaza visa vipya vya wagonjwa wanaogundulika kuwa #CoronaVirus, badala yake itangaze idadi ya watu wanaopona na idadi ya wanaofariki.
Mwigulu amesema hayo jana Jumanne Aprili 14 , 2020, wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi)
“Mimi ninawaza serikali itoe taarifa za aina tatu tu kuhusu wagonjwa wa corona, tutoe taarifa ya wagonjwa wapya, taarifa ya wagonjwa waliopona na pengine kwa bahati mbaya sana wagonjwa waliokufa.
“Isiwe kama tunashindana kwa idadi ya wagonjwa na nchi nyingine, kwamba ‘tume-develop’ wagonjwa wengi, hiki kitu hakijakaa sawa, sijui kwa nini wengi wanatamani idadi iwe kubwa. Kama Mungu ameamua kutunusuru kwani nyinyi mna kikao na Mungu? Mna-debate na Mungu? Kwa nini mnataka wagonjwa waongezeke? Watanzania tubadili mitazamo kuhusu jambo hili,” amesema Mwigulu.
