×

Mazishi ya Mzee wa Miaka 100 Aliyejengea Shule Watoto Wake – Video

MWILI wa marehemu Mzee Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laibon, mkazi wa wilayani Monduli mkoani Arusha aliyekuwa na umri zaidi ya miaka 100 amezikwa jana Jumatano, Aprili 15, 2020, nyumbani kwake wilayani humo.

Mzee Laibon alikuwa maarufu kiasi cha kuwafanya watu kutoka mataifa ya nje kuja nchini kumshuhudia kama sehemu ya utalii hasa kutokana na mzee huyo ambaye alikuwa Mmaasai kuanzisha shule yake na soko kwa ajili ya watoto wake, wajukuu zake na ukoo wake kwa ujumla.

 

Mzee huyo, enzi za uhai wake alikuwa na wake nane na watoto 54, pamoja na wajukuu 81 lakini pia alikuwa na nyumba zaidi ya arobaini ambazo jamii yake ilikuwa ikiishi hapo.

 

Leave a Comment