×

Uchumi wa China Washuka kwa Asilimia 6.8, Kisa Covid-19

UCHUMI wa China umeshuka kwa asilimia 6.8 katika robo ya kwanza ya mwaka kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa kutokana na viwanda na biashara mbalimbali kufungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

 

China ambayo uchumi wake unashika nafasi ya pili duniani una nguvu kubwa katika uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali za mlaji duniani.

 

Hii ni mara ya kwanza uchumi wa china unashuka katika miezi mitatu ya mwaka tangu ulipoanza kuwa na nguvu kubwa katika vipindi kama hivyo tangu mwaka 1992.

 

Mwaka jana uchumi wa China ulifikia ukuaji wa asilimia 6.4 katika robo ya kwanza ya mwaka, kipindi ambacho ilikuwa katika ushindani mkubwa na Marekani kibiashara.

 

Katika miaka 20 iliyopita, China imeshuhudia uchumi wake ukikua kwa wastani wa asilimia 9 kwa mwaka, licha ya wataalam kutilia mashaka usahihi wa takwimu hizo.

 

Uchumi wake umeshuka katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya mwaka kutokana na watu kufungiwa katika makazi yao na karantini mbalimbali kwa ajili ya kuzuia kunea kwa virusi hivyo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu.

Leave a Comment