MWANAMUZIKI sexy wa Bongo Fleva, Maua Sama ameweka wazi juu ya ombi lake la kupata mchumba mwenye mapenzi ya kweli.
Baada ya kuposti bango hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, IJUMAA lilimtafuta Maua na kupiga naye stori juu ya jambo hilo na ishu nyinginezo;
IJUMAA: Baada ya kuposti ujumbe wa kuomba upate mchumba mwenye mapenzi ya kweli na kama ana pesa ampelekee mama’ke, baadhi ya mashabiki wako wamedai umeishiwa ndiyo maana unataka mwanaume yeyote hata asiyekuwa na pesa, je, hilo unalizungumziaje?
MAUA SAMA: Kuzungumziwa vibaya mimi nilishazoea, huwa hainishtui na siwezi kuwazuia watu kuongea mitazamo yao na huwa napokea kila mawazo ya mtu.
IJUMAA: Sasa katika hili ambalo umeliposti, ni kwamba unatafuta kiki ya kutoa wimbo mpya au ni kweli unatafuta mchumba?
MAUA SAMA: Posti za Instagram huwa naposti kila siku. Mara nyingi napenda kuchati na kuwa karibu na mashabiki wanaofuatilia kazi zangu za muziki, so huwa naposti wakati wote hata kama sina plani za kutoa wimbo. Nyimbo zipo nyingi, wakati ukifika tutainjoi muziki mzuri. Nawapenda sana watu wangu na waendelee kunisapoti.
IJUMAA: Je, una mchumba na kama unaye tutarajie ndoa lini?
Maua Sama: Mimi ni binadamu kama binadamu wengine, natamani nije kuwa na mume wangu na sipendi kutendwa kwa kuwa huwa naumia. Nina matamanio pia kwa hiyo naweza kutamani ndoa na mtoto pia. Lakini kila kitu kinapangwa na Mwenyezi Mungu.
IJUMAA: Ungetamani mume wako awe ni mtu wa aina gani?
MAUA SAMA: Natamani mume wangu awe muelewa na mwenye mapenzi ya dhati na zaidi sana awe mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu.
IJUMAA: Vipi mashabiki wako wanatamani kuona unatoka na kuufikisha muziki wako mbali kidunia maana ni kitambo upo kwenye gemu, unawaambiaje?
MAUA SAMA: Sipo muda mrefu sana kwenye muziki kama inavyotafsiriwa. Mara zote huwa naamini ndiyo kama naanza na nahitaji kufanya vitu vizuri.
Mashabiki wangu wawe tayari. Kuhusu mipango ya kimataifa, kuna projekti kadhaa nimefanya na naendelea kufanya ili kufikia malengo yangu ya kuufanya muziki wa Tanzania kutambulika zaidi. Wandelee kunifuatilia kwenye chaneli zangu za mitandao ya kijamii.
Stori: Neema Adrian, Dar
