×

Shilole Profile: Kuzaliwa, Elimu, Uigizaji, Mfanyabiashara -Video


Zuwena Yusuph Mohammed (anayejulikana kwa jina lake la kisanii kama Shilole au “Shishi Baby” na Shishi Trump; amezaliwa 20 Disemba 1987) ni msanii wa maigizo na muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania.

Alianza kupata umaarufu baada ya kucheza filamu ya “Fair Decision” (2010) ambayo ndani kacheza na Vincent Kigosi (Ray), Irene Uwoya, Mwanaidi Suka, Blandina Chagula, Jennifer Kyaka na Jacob Stephen (JB). Filamu zingine ni pamoja na Don’t Play, Chungu ya Nafsi, Curse of Marriage, Zawadi ya Birthday na Talaka Yangu. Mbali ya muziki na uigizaji Shilole vilevile ni mjasiriamali anayejishughulisha na biashara ndogondogo na za mama ntilie. Jambo ambalo sio rahisi kwa wasanii wengi wa maigizo wa Tanzania. Mgahawa wake unaitwa “Trump Food”.

Leave a Comment