×

Ccm Dar, Kugawa Bure Barakoa Milioni 1

Kate Kamba akionesha mfano wa barakoa hizo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba amesema ofisi yake imedhamiria kugawa bure barakoa milioni moja kwa ajili kupambana na Ugonjwa wa Covid-19 unaoenezwa na virusi vya corona.

 

Kate alisema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kwenye Makao Makuu ya chama hicho mkoa wa Dar es Salaam.

 

Akizungumza na wanahabari Kate alisema anamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kulisisitiza taifa kufunga na kumuomba Mungu ili atuepushe na janga corona.

Kate akiwa na viongozi wenzake wa mkoa kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti huyo alimsifu Rais Magufuli kwa kuendelea kuwasisitiza wananchi kufanyakazi na kuwataka waishi kwa tahadhali.

 

Katika kupambana na ugonjwa huo Kate amesema ofisi yake inatarajia kugawa bure barakoa milioni kwa wananchi ambazo watazitengeneza wenyewe zikiwa na ubora wa hali ya juu ili kuwaokoa wasiokuwa na uwezo wa kuzinunua.

 

Mwenyekiti huyo ameelezea kusikitishwa kwake na wafanyabiashara walifanya janga hilo kuwa mradi na kuwauzia wananchi barakoa hizo kwa bei ya juu kuanzia 1000 mpaka 3500.

 

“Nawaomba Wafanyabiashara wawe na ubinaadamu na wasitumie ugonjwa huu kutaka kujinufaisha kwa kuuza barakoa kwa bei ambazo mwananchi wa kawaida ni ngumu kuimudu,” alimaliza kusema Mwenyekiti huyo.

 

HABARI:NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

 

Leave a Comment