×

Wafungwa Waliosamehewa na JPM Handeni Waachiwa – Video

BAADA ya Rais John Magufuli kutangaza msamaha kwa wafungwa 3,973 nchini, Wilaya ya Handeni imekuwa miongoni mwa wilaya za kwanza kutekeleza maelekezo hayo ambapo jumla ya wafungwa 38 kati yao 13 wameachiwa huru huku wengine 25 wakipunguziwa adhabu.

 

Wakiongea wakati wa kutoka gerezani wafungwa hao wamemshukuru rais kwa msamaha aliowapatia  wakiahidi kuwa raia wema ndani ya jamii na baadhi yao wakisema kuwa kupitia gereza hilo wamejifunza vitu vingi ikiwemo stadi za maisha pamoja na shughuli mbalimbali za uzalishaji hasa kilimo.

 

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe,  pamoja na kuwataka wafungwa hao kuwa raia wema pia akawasisitiza wanapokwenda wazingatie tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Msamaha huo uliotolewa na rais katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment