MY Style ni kolamu ambayo inakuletea maisha ya nje ya sanaa ya mastaa mbalimbali. Leo tupo na mwanadada ambaye ameamua kupiga ndege wawili kwa jiwe moja katika muziki na filamu, si mwingine bali ni Baby Joseph Madaha ambaye alishawahi kutamba na ngoma kama Amore na nyingine nyingi.
Amezungumza mengi hususan yale yahusuyo mitindo ya maisha:
My Style: Ratiba yako unapoamka iko vipi?
Baby Madaha: Kwanza kabisa nafanya mazoezi ya mwili, nakunywa maji ya moto, naoga halafu nakunywa pombe, ndiyo inayonibusti katika kazi zangu.
My Style: Watu wengi wanapendelea kunywa chai asubuhi, wewe uko tofauti kwa nini?
Baby Madaha: Ninapokunywa pombe nachangamka sana, pia akili yangu inakuwa sawa.
My Style: Unapendelea kunywa pombe ya aina gani?
Baby Madaha: Pombe kama za Wazungu zile zinaitwa liquid kwa jina la Kizungu, ambazo ni aina ya whisky, maana pombe za Kibongo zinazeesha tu.
My Style: Chakula gani ambacho kilishawahi kukupa changamoto katika kukipika?
Baby Madaha: Mimi napenda sana Mandi, chakula cha kihindi na kinanipa changamoto hadi leo katika kukipika, yaani ni kigumu aisee.
My Style: Unapotoka na mpenzi wako, unapenda awe katika muonekano gani?
Baby Madaha: Napenda avae sweta au nguo ya mikono mifupi na pensi fupi kwa sababu ana mwili mzuri sana, hapo ndiyo naona amependeza.
My Style: Mkitoka mnapendelea kwenda maeneo gani kula bata?
Baby Madaha: Mimi ni mpenzi wa kwenda beach, lakini yeye anapenda twende mtaani tule vyakula vya mtaani, awe na marafiki zake hapo ndiyo anaenjoy.
My Style: Unapokuwa nyumbani, unapendelea kufanya nini?
Baby Madaha: Napenda nicheze na mpenzi wangu, nimpikie chakula ninachokipenda na mara nyingi napenda kupika ndizi nyama kwa sababu ndiyo anapendelea.
My Style: Unapokuwa naye unapenda kumfanyia kitu gani?
Baby Madaha: Napenda kumbusu na kulalia kifua chake.
My Style: Katika simu yako, umemsave vipi na yeye kakusave vipi?
Baby Madaha: Nimemsave Hubby kwa yeye sijui kanisave vipi, mwanzo alinisave Baby Madaha kwa sasa hivi sijui.
My Style: Ni kitu gani anakipenda zaidi kutoka kwako?
Baby Madaha: Anasemaga anapenda sana kifua changu jinsi kilivyo, kiko sexy kabisa.
My Style: Nguo gani ukivaa unaona uko comfortable kabisa?
Baby Madaha: Inategemea na sehemu ninayoenda, ila mara nyingi napenda nguo za hewa na ziwe fupi, hapo nakuwa sawa.
My Style: Ni rangi za aina gani ambazo unapendelea?
Baby Madaha: Napenda rangi nzito kama nyeusi, nyekundu au bluu, sipendi mwanga, maana hata nyumbani kwangu naweka taa nyekundu au bluu.
My Style: Kitu gani ambacho huwezi kutoka bila kukivaa kati ya bangili, cheni au pete?
Baby Madaha: Siwezi kutoka bila pete au bangili yaani hapo lazima nirudi kuvaa.
My Style: Ni kitu gani ambacho ukifanyiwa unaonyesha hasira zako?
Baby Madaha: Kudharauliwa au mtu kunifokea, yaani huwa sipendi na ikitokea hivyo nakwazika sana kwa muda huo.
My Style: Katika pochi yako, haviwezi kukosekana vitu gani?
Baby Madaha: Perfume, chaji ya simu, make up na pesa kidogo.
My Style: Ni aina gani ya kiatu ukivaa unajiona mrembo zaidi?
Baby Madaha: Napenda sana snickers, na viatu virefu japo mara nyingi huwa navaa nikiwa shooting baada ya hapo navua.
My Style: Unawaambia nini mashabiki zako?
Baby Madaha: Nawapenda, waendelee kufuatilia kazi zangu.
Baby Madaha: Napenda nicheze na mpenzi wangu, nimpikie chakula ninachokipenda na mara nyingi napenda kupika ndizi nyama kwa sababu ndiyo anapendelea.
MAKALA: HAPPYNESS MASUNGA
