MAZIKO ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, yamefanyika asubuhi ya leo, Aprili 28, 2020, eneo la Pemba Mvita na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.
Mmanda alifariki dunia alfajiri ya jana (Jumatatu), Aprili 27, 2020, katika Hospitali ya Ligula, Mtwara, kutokana na maradhi ya moyo na maziko hayo yamehudhuriwa na ndugu wachache na kusimamiwa na serikali.
Mmanda aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Rais John Magufuli, Desemba 19, 2016, akichukua nafasi ya Dkt. Khatib Kazungu ambaye alihamishiwa Wizara ya Fedha.
Wakili msomi Mmanda aliyekuwa pia mjumbe wa Bunge la Katiba, katika bunge hilo, aliteuliwa na Mwenyekiti wa muda wa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho, kuwa mmoja wa wajumbe 20 ambao walimshauri ili kuboresha utendaji.
Aidha, mwaka 2015 Mmanda alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Rombo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini kura hazikutosha.
Na Edwin Lindege | GPL


