×

Lyyn Adaiwa Kufuata Nyayo za Mobeto kwa Kiba

JUZIKATI f’lani hivi, huyu video vixen na msanii wa Bongo Fleva, Irene Louis ‘Lyyn’ aliibua stori nyingi kama kawaida yake.

 

Ilisemekana kwamba, wakati staa mwenzake, Hamisa Mobeto anatrendi na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kutokana na Ngoma ya Dodo, naye zilipenya tetesi za motomoto kwamba anatoka kimapenzi na jamaa huyo.

 

Inafahamika kwamba, Lyyn ni zilipendwa wa staa mwingine wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni hasimu wa Kiba, hivyo tetesi hizo zilikuwa ‘pambe’.

Katikati ya mvurugano huo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limefanya mahojiano maalum (exclusive) na Lyyn kutaka kujua kuna nini nyuma ya pazia ambapo amefunguka anachokijua.

 

IJUMAA WIKIENDA:

Siku hizi huonekani sana kwa sababu ya Corona. Je, unafanya nini kwa sasa?

LYYN: Ni kweli sionekani kwa sababu ya Corona. Imebidi nikae tu nyumbani na kuepuka safari zisizokuwa za lazima.

 

IJUMAA WIKIENDA: Lakini inasemekana siku hizi warembo wengi hamuonekani mjini kwa sababu ‘masponsa’ wapo bize na familia zao!

LYYN: Hapana, siyo kweli, kwani kuna mtu haogopi Corona?

IJUMAA WIKIENDA: Je, ni kweli nyumba uliyopanga kwa sasa Masaki (Dar) unalipa zaidi ya shilingi milioni tatu kwa mwezi?

 

LYYN: Ndiyo, huo ndiyo ukweli!

IJUMAA WIKIENDA: Shilingi milioni 3 kwa mwezi mmoja ni pesa nyingi sana hasa katika kipindi hiki kigumu tulichonacho, kwa nini usijenge nyumba yako?

LYYN: Nina nyumba nyingi sana, lakini nyumba ambayo nataka mimi kuishi, bado haijamalizika hivyo nasubiria imalizike kisha nihamie.

 

IJUMAA WIKIENDA: Umesema una nyumba nyingi, zipo ngapi na wapi?

LYYN: Wewe jua tu ni nyingi. Kuna nyingine zipo Kigamboni (Dar) nimeweka wapangaji na pesa yao ya kodi ndiyo ninatumia kupangisha nyumba, kuweka magari mafuta na nyingine ndizo natumia kumalizia kujenga nyumba ninayotaka kuishi.

 

IJUMAA WIKIENDA: Wasanii wengi wanategemea shoo na vitu vingine kwa ajili ya kuendesha maisha, lakini mikusanyiko imepigwa ‘stop’ kwa sababu ya Corona, hali hii imekuathiri kiasi gani?

LYYN: Kwanza nilikuwa nataka kutoa EP (albam fupi), halafu nilikuwa nahitaji kushuti video mpya, lakini vyote hivyo vimeshindikana kwa sababu ya Corona.

IJUMAA WIKIENDA: Wasanii wengi sasa hivi mmejikita kwenye kutoa EP, vipi mipango ya albam?

LYYN: Nimepanga kutoa albam mwakani.

 

IJUMAA WIKIENDA: Kabla ya kutoa hiyo albam, umejifunza nini kutoka kwa wasanii waliokutangulia waliotoa albam kama Vanessa, Diamond, Harmonize na wengineo?

LYYN: Nimejifunza mambo mengi sana na bado nazidi kujifunza, hivyo naamini nitatoa kitu kizuri.

IJUMAA WIKIENDA: Baadhi ya wasanii kipindi hiki cha Corona wanaachia nyimbo zao kwa mfumo wa audio tu, vipi kwa upande wako umepanga kufanya nini ili mashabiki wako wasikusahau?

 

LYYN: Kuachia audio ndiyo mpango wangu. Nitatoa audio ya wimbo mpya hivi karibuni.

IJUMAA WIKIENDA: Kuna tetesi kuwa ulimfuata Kiba ofisini kwake na kumuomba kolabo au kufanya naye kitu kama alivyofanya na Mobeto, lakini akakutolea nje. Je, ni kweli?

 

LYYN: Siyo kweli. Nilikwenda ofisini kwake kwa ishu zangu nyingine kabisa wala siyo kwa sababu hiyo. Hata mimi nimeshangaa kusikia eti nilikwenda kuomba kolabo kwa Ali (Kiba), jambo ambalo si kweli. Nina uhakika hata Ali (Kiba) mwenyewe ameshangaa kwa sababu hata siku hiyo hatukuonana kabisa.

 

IJUMAA WIKIENDA:

Kwani hujawahi kutamani kufanya naye kolabo?

LYYN: Natamani sana na napenda kwa sababu ni mwanamuziki mkubwa. Nadhani siku moja uongozi wangu utamtafuta na naamini tutafanya jambo.

 

IJUMAA WIKIENDA: Ni kweli kwamba unatoka naye kimapenzi?

LYYN: Hapana, sasa jamani mtu sijawahi hata kuonana naye nitatokaje naye kimapenzi?

IJUMAA WIKIENDA: Unamaanisha hujawahi kuonana kabisa na Kiba?

 

LYYN: Nimewahi kumuona mara moja, tena kwa mbali, lakini hatujawahi kukutana na kuzungumza chochote.

IJUMAA WIKIENDA: Ni mafanikio gani ambayo umeyapata tangu uanze kufanya muziki?

LYYN: Muziki umenisaidia japo siwezi kusema sana, lakini kuna vitu nikiangalia nasema hivi vimetokana na muziki.

 

IJUMAA WIKIENDA: Una neno lolote kwa mashabiki wako?

LYYN: Nawapenda sana, naomba waendelee kusapoti kazi zangu.

MAKALA: Memorise Richard

Leave a Comment