WAKILI maarufu wa kujitegemea, Alberto Msando, ametoa msaada wa barakoa 100 pamoja na vitakasa mikono 100 kwa waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa Covid-19 unaotokana na virusi vya corona.
Akikabidhi msaada huo jana kwenye ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) kupitia kwa mwenyekiti wa chama hicho, Claud Gwandu, Msando alisema wanahabari ni watu muhimu katika kuandika na kupambana na ugonjwa huo.
Alisisitiza kwamba wanahabari ni watu muhimu katika kutoa taarifa sahihi za kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kuelimisha jamii juu ya maambukizi ya ugonjwa huo na kuhakikisha wanafuata taratibu zote zinazotakiwa katika kujikinga dhidi yake.
Naye Mwenyekiti wa APC, Gwandu alishukuru kwa msaada huo ambao utawasaidia kujikinga na ugonjwa huo na kutoa rai kwa wadau wengine kujitoa kusaidia wanahabari katika kupambana na ugonjwa huo.
Wanahabari wengine wa Mkoa wa Arusha: Lillian Joel wa gazti la Uhuru na Cynthia Mwilolezi wa Nipashe walishukuru kwa msaada huo ambao utawasaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
