×

Video: Rais Magufuli Aagiza Dawa ya Corona Madagascar


Rais Dkt. John Magufuli leo Mei 3, 2020 amesema amefanya mawasiliano na nchi ya Madagascar ambayo imegundua dawa ya CORONA na kusema serikali inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha inaishinda vita dhidi ya CORONA.

 

Rais Magufuli amesema atatuma ndege kwenda nchini humo kuchukua dawa ya CORONA ili ije kuwasadia Watanzania.

 

Ameyasema hayo wakati akimuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye alifariki dunia jana na kuzikwa leo nyumbani kwao mkoni Iringa. Rais Magufuli ameendelea kuwasisitiza wananchi kwamba wasiogope na kuwataka viongozi wa dini kusimama imara katika kipindi hiki kigumu.

Leave a Comment