×

Baba D Ampigia Saluti Mondi

 

DAR: Baada ya Diamond Plutnumz kuonyesha karatasi aliyolipia familia za watu 500 kulipia kodi za nyumba kwa muda wa miezi mitatu kipindi huki cha ugonjwa Wa Corona, baba ake mzazi Abdul Juma amempongeza na kusema kuwa aendelee na moyo huwo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda Baba D alisema kuwa yeye anampongeza kwa kuwa amesaidia familia zenye uhitaji.

 

“Mimi nimempongeza kwa kitendo alichokifanya sasa watu wanasema hanisaidii Mimi anasaidia watu wengine Mimi nina nyumba yangu ninaishi silipi kodi ile ilikiwa kwa wale watu ambao wamepata changoto kipindi hiki cha Corona huenda walikuwa hawana uwezo Wa kulipa kodi ndio maana amejitolea kuwalipia.

 

“Kwa hiyo Mimi nampongeza na aendelee kuwa na Moyo Wa kusaidia ingawa kuna watu huwa wanamkatisha tamaa yeye asiwasikilize,”alisema Baba D.

Stori: INEEMA ADRIAN, IJUMAA Wikienda

Leave a Comment