PAUL Nonga, nahodha wa Klabu ya Lipuli, amesema kuwa kwa sasa amesepa ndani ya mkoa wa Iringa na kujichimbia Mbeya akiwa na familia yake.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Nonga alisema kuwa aliondoka Iringa yalipo makao makuu ya timu ya Lipuli baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona.
“Nimeondoka Iringa kwani kambi tulivunja kutokana na janga la Corona, kwa sasa nipo Mbeya na familia yangu tukiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
“Wakati huu mgumu kila mmoja anapaswa kuendelea kujilinda mwenyewe pamoja na jamii inayomzunguka ili kulishinda hili janga ambalo limekuwa ni tishio kwa dunia nzima,” alisema Nonga mwenye mabao 11 na pasi nne za mabao.
Stori na Lunyamadzo MLyuka