×

Gavana Kenya Apiga Marufuku Uuzaji Ng’ombe wa Tanzania

GAVANA wa Kajiado, Joseph Lenku, amefunga kabisa uuzaji wa ng’ombe katika kaunti hiyo kutoka Tanzania kutokana na visa vya maambukizi ya COVID-19 yanayoripotiwa Tanzania.

 

Lenku ametoa amri hiyo baada ya kufanya ziara eneo la Loitoktok ambapo alikuwa anasambaza barakoa kwa wakazi wa kaunti hiyo waliomkashifu kwa kutozuia mapema uuzaji wa ng’ombe eneo hilo kutoka Tanzania.

 

Soko Kuu la Bissili linaloshirikisha Athi River na mpaka wa Namanga lilikuwa bado linakubali wauzaji wa ng’ombe kutoka Tanzania kabla ya kufungwa.

 

Hatua ya maambukizi kuongezeka nchini Tanzania iliwatia hofu idadi kubwa ya Wakenya hasa wanaoishi karibu na mipaka ya mataifa haya mawili kama vile Loitoktok, Namanga, Shompole na karibu na Ziwa Natron.

 

Leave a Comment