×

Mbunge Aliyetangazwa Kuwa na #Coronavirus Anaendelea Vizuri

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Mbunge aliyetangazwa kuwa na maambukizi ya #CoronaVirus mwezi uliopita anaendelea vizuri na anasubiri vipimo vya mwisho ili aruhusiwe.

 

Kwa mujibu wa Spika Ndugai, Mbunge huyo hakuugua magonjwa ya dalili za #COVID19 lakini alikutwa na Virusi vya Corona.

 

Mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson alitangaza kuwa Mbunge mmoja amekutwa na maambukizi ya #COVID19.

 

Leave a Comment