×

Kisa Corona, Niyonzima Amvuta Kaseja

Haruna Niyonzima.

KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amelazimika kuwavuta kwenye mazoezi ya pamoja wakongwe wenzake, Juma Kaseja na Shabani Kado, ikiwa ni mkakati mahususi wa kujiandaa na tamko la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) la kurejea kwa Ligi Kuu Bara.

 

Kufuatia kuwepo na taarifa za TFF kuwa katika mipango ya ndani ya kuirejesha ligi hivi karibuni, baadhi ya wachezaji kutoka klabu mbalimbali kama Juma Kaseja anayeipigia KMC, Shabani Kado wa Mtibwa Sugar na Niyonzima pamoja wameamua kuongeza muda wa mazoezi yao ya kila siku ikiwa ni mpango mahususi wa kujiweka sawa.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Niyonzima alisema kuwa, awali baada ya ligi kusimamishwa alikuwa akifanya mazoezi mara moja kwa siku nyumbani kwake kama alivyokuwa amepangiwa na kocha wake, Luc Eyamel, lakini kwa sasa ameungana na Kaseja na Kado ambapo wanafanya mara mbili kwa siku.

“Awali nilikuwa nafanya kweli mazoezi mara moja tena nyumbani maana kuna nafasi ya kutosha ambayo ilikuwa inaniwezesha kwendana na program za kocha, ila siku zinavyoenda nimelazimika kuongeza muda wa mazoezi ambapo sasa hivi nafanya na Kaseja pamoja na Kado.

 

“Mazoezi yetu mara kadhaa tunafanyia katika ufukwe wa Escape One pale Mikocheni na tumekuwa tukijitahidi sana kufanya mazoezi ambayo yanaweza kutufanya tuendelee kuwa na utimamu sahihi wa mwili ili hata kama zile taarifa za ligi kurejea zikikamilika basi zitukute tuko fi ti,” alisema Niyonzima.

Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam

Mbunge JAMES MBATIA kuhusu CORONA, LOCKDOWN, Afunguka CHADEMA Kutoingia BUNGENI | GLOBAL RADIO

Leave a Comment