×

WHO: Waafrika 190,000 Wanaweza Kufariki kwa #Coronavirus

SHIRIKA  la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa #CoronaVirus unaweza kusababisha vifo kwa Waafrika wapatao 190,000 ndani ya mwaka mmoja tangu uanze, kama ukishindwa kudhibitiwa.

 

Mkurugenzi wa WHO-Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amesema kuna uwezekano kuwa #COVID19 haitosambaa kwa kasi barani humo kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine duniani.

 

Hata hivyo, amezitaka Serikali kuweka mikakati ya kupima #Corona, kuwatibia wagonjwa, kuweka wenye maambukizi karantini na vilevile kutafuta wale waliokuwa karibu na wagonjwa wa virusi hivyo.

 

Awali, WHO ilitabiri Waafrika Milioni 29 hadi 44 wanaweza kupata #COVID19 kwa mwaka mmoja na Milioni 5.5 wanaweza kuhitaji tiba Hospitali, idadi ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa sekta za afya katika nchi nyingi.

Leave a Comment