×

Nicole Avuruga Penzi La Harmo na Sarah

KAMA hufahamu, mrembo Nicole Joyberry anayejinasibu kuwa ni mkulima wa matikiti mkoani Iringa, ametibua penzi kati ya msanii Rajabu Abdul ‘Harmonize’ au Harmo na Sarah Michelotti.Kilanga chote cha mtifuano wa wawili hao ambao wamekuwa wakitaka watambuliwe kuwa mke na mume, kilianzia Instagram ambako Harmo ndiyo alikuwa wa kwanza kuchachua utamu.

 

ILIKUWA HIVI!

Katikati ya wiki hii Harmo aliingia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kujiweka live kupitia video na kisha kumwalika Jackline Wolper (mpenziwe wa zamani) na video queen, Nicole aliyempambia video ya wimbo wake wa Bedroom kisha kuanza kupiga nao stori.

 

Ni wazi kuwa Harmo alifahamu kuwa mpenzi wake Sarah atachungulia mahojiano hayo, lakini kibishi hakujali na hivyo kumpa nafasi Nicole kutumia nafasi hiyo kujisafisha na skendo ya kutoka na Harmo huku akimtaka Sarah kuwa na amani.Kujisafisha huko kunatokana na Nicole kuchafua hali ya hewa hivi karibuni baada ya wimbo wa Bedroom ambapo Sarah alimtuhumu kutoka na Harmo wakati wakitengeneza video ya wimbo huo na hivyo kuzua tafrani fulani ‘ameizingi’.

SARAH ALIVYOIBUKA

Wakati Nicole akijitakasa laivu sijui kwa kutumia sabuni au sanitaiza kwenye video ya Istagram ya Harmo iliyokuwa ikiruka bilachenga, Sarah aliibuka na ujumbe huu mzito:“Baby (Harmo) nenda (sijui wapi) salimia Nicole nyumbani, Byeee usiku mwema.”Mwanadada huyo hakuishia hapo alimalizia na bonge la tusi ambalo kiukweli haliandikiki gazetini.

Baada ya ujumbe huo mzito kumfikia Nicole, naye akaona siyo ishu akaibuka na kujibu shiti na kufanya mambo yakorogeke zaidi.

Baada ya kuona supu inazidi kutiwa nazi, wapambe nuksi waliokuwa wakifuatilia video hiyo ya laivu walianza kukomenti kati yao wengine wakimshambulia Harmo kwa kumtaja kuwa ni mtu aliyedhamiria kumdhalilisha mkewe hadharani.Hata hivyo, wenzake na bibie huyo walichukulia poa na kutaka ulingo uendelee ili wazidi kupata vionjo vya michambo kuntu.

 

“Yaani huyu Harmo hapana jamani, sasa kulikuwa kuna haja gani ya kuingia Insta live na wanawake zake wa zamani? Hiyo siyo heshima hata kidogo, amemdhalilisha sana mke wake, ningekuwa mimi ndiyo Sarah ningetulia tu hata hiyo live nisingeenda.

Yaani nisingejaribu hata kujibishana na mdangaji wa mjini, ningekumbatia huba langu,” alikomenti mdau mmoja aliyefahamika kwa jina la @mrs-J.Habari za chini ya kapeti zinaeleza kuwa tangu hapo uhusiano kati ya Harmo na Sarah mwenye asili ya Kiitaliano, ni kama unapumulia mashine na chanzo kililiambia gazeti hili kuwa moto unafukuta chini kwa chini.

 

Mara kadhaa meneja wa Harmonize, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ amekuwa akiulizwa kuwepo kwa mgogoro wa kimapenzi kwa wawili hao kwa sababu ya Nicole, amekuwa akikanusha na kusema kwenye uhusiano migogoro ni jambo la kawaida.

 

Wiki chache zilizopita baada ya kusambaa mitandaoni video ikisikika sauti ya Sarah akimfokea Harmo kwa kile kilichotajwa kuwa ni usaliti wake kwa Nicole, gazeti dada la hili Ijumaa Wikienda lilimuuliza Beauty kinachoendelea kati ya wawili hao ambapo alisema: “Jamani kwani hamjui kuwa Sarah na Harmo ni mke na mume? Ile ni familia hivyo kama ikitokea hawajaelewana, Sarah ana uwezo wa kumfokea mume wake,” alisema meneja huyo.

 

Alipotafutwa Nicole hivi karibuni ili azungumzie skendo ya kutoka na Harmo, alisema:“Unajua kilichonikutanisha mimi na Harmo ni kazi, na tulifanya kazi tena nilijitolea tu maana hakunipa hela yoyote ile, isitoshe tulilala Appartment moja kwa siku tatu na hatukufanya kitu chochote. Sasa nashangaa kuambiwa natoka naye.

STORI: MEMORISE RICHARD, RISASI

KIJANA MTANZANIA ALIYEBUNI SILAHA YA CORONA, AMLILIA RAIS MAGUFULI | PART 1

Leave a Comment