Burundi yamtimua toka nchini humo mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na wataalamu watatu wa afya wa shirika hilo. Burundi imesema maafisa hao wameingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo na kuacha kufuata mwongozo wa mahusiano kati ya WHO na Burundi.
