Mkurugenzi Mtendaji wa Programu za Dharura za Afya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Mike Ryan amesema Corona Virus vinaweza vikaendelea kuwepo na kujiunga na mchanganyiko wa virusi vingine vinavyoendelea kuua watu duniani.
Ametolea mfano virusi vya UKIMWI ambavyo hadi leo vipo akisema hafananishi virusi hivyo ila ni vyema watu kujua uhalisia, kwa kuwa hakuna anayeweza kutabiri siku ambayo #COVID19 inaweza kuondoka.
Amesema chanjo inaweza kupunguza madhara ya #CoronaVirus, lakini chanjo inapaswa kuwepo na kuwa na ufanisi wa hali ya juu na kupatikana kwa kila mtu duniani.
