×

Sheva Arudi Kibabe, Azuia Usajili Simba

KUREJEAkutoka kwenye majeraha kwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Miraji Athuman ‘Sheva’ kumezuia usajili wa kiungo wa Polisi Tanzania, Sixtus Sabilo na Lucas Kikoti anayekipiga Namungo FC.

 

Kikoti na Sabilo ni kati wa viungo washambuliaji wanaotajwa kutakiwa na Simba kwenye msimu ujao katika kuiboresha safu ya kiungo ya timu hiyo inayoongozwa na Luis Miquissone, Francis Kahata, Hassani Dilunga, Deo Kanda, Shiza Kichuya na Sheva mwenyewe.

Simba chini ya mwekezaji wake bilionea, Mohammed Dewji, imepanga kufanya usajili wa kufuru katika kuelekea msimu ujao kama ilivyokuwa kwa Yanga iliyokuwa chini ya wadhamini wake Kampuni ya GSM.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Soti Xtra, Simba imepanga kufanya usajili wake kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji ambazo ndiyo zimeonekana kuwa na upungufu mkubwa.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa safu ya kiungo hawaifi kirii kwa hivi sasa na hiyo ni kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza nafasi hiyo kati ya hao wapo wanaomaliza mikataba yao ambao wamepanga kuwaongezea.

 

“Tuna idadi kubwa ya viungo wachezeshaji na washambuliaji katika timu yetu, labda kama tukiongeza ni kiungo mkabaji pekee yenye wachezaji wawili ambao ni Jonas Mkude na Mzamiru Yassin.

 

“Nguvu kubwa tumeeleka katika kuiboresha safu ya ulinzi na ushambuliaji pekee, kwani ndiyo ambazo kocha ameziona zina upungufu katika msimu huu.

 

“Ngumu kusajili viungo wakati wapo wengi katika timu na tayari Sheva amepona na ameanza mazoezi magumu na mepesi ufukweni kwa ajili ya kujiweka fi ti. Tunatarajia kumuona baada ya ligi kuanza,” alisema mtoa taarifa huyo.Sheva alithibitisha hilo kwa kusema kuwa: “Nipo fi ti hivi sasa kurejea uwanjani na subirieni kumuona Sheva mpya akirejea.

STORI: WILBERT MOLANDI, CHAMPIONI

Leave a Comment