×

Trump: Sitaki Tena Mazungumzo na China

UHUSIANO kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota kwa kasi tangu kuanza kwa jana la Corona lililoua makumi ya raia wa Marekani.

 

Jana, Mei 14, 2020 , Rais wa Marekani, Donald Trump, alisema kwa sasa hana mpango na hataki kuzungumza na Rais Xi Jinping wa China na akaenda mbali zaidi na kusema anafikiria kusitisha uhusiano na taifa hilo la pili kwa nguvu za uchumi duniani.

 

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Fox, jana, Trump alisema amesononeshwa  na kitendo cha China kushindwa kulidhibiti janga la corona.

 

Takwimu zinaonesha Marekani imeathiriwa vibaya zaidi na virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Kwa takwimu za leo asubuhi, maambukizi ya virusi vya corona nchini humo yamefika 1,457,593, waliopona ni 318,027 na vifo vimefika 86,912.

 

Leave a Comment