
JUVENTUS inamtaka Arthur Melo katika dili la kubadilishana na Miralem Pjanic kutua Barcelona. Wakati hayo yakijiri, Barcelona imesema haipo tayari kumlazimisha kiungo wake huyo kutimkia Juventus kama mwenyewe hataki kwenda.
Hivi karibuni, Arthur alinukuliwa akisema: “Ninataka kuendelea kuwa hapa Barcelona. Kichwani mwangu sina chaguo lingine zaidi ya hapa nilipo.”
Kiungo huyo ambaye ameonekana kutokuwa na nafasi msimu huu ndani ya Barcelona, inaelezwa kuwa yupo kwenye mipango ya msimu ujao na klabu hiyo.
BARCELONA, HISPANIA