×

Mshindi Toboa Kimuziki na Global TV Anyakua Tuzo!

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa awamu ya kwanza ya lile shindano kubwa la kuinua vipaji vya muziki nchini lililokuwa likiendeshwa na kituo cha Global TV Online imefikia tamati leo Jumatatu, Mei 18, 2020, huku msanii chipukizi, Goweshan  akiibuka mshindi na kujinyakulia tuzo.

Shindano hili lilizinduliwa rasmi Machi 12, 2020 na lilikuwa na jumla ya washiriki kumi ambao video zao zilikidhi vigezo kuingia kwenye shindano, lengo kubwa likiwa ni kuwapa fursa vijana chipukizi ambao hawana wa kuwashika mkono kwenye safari yao ya kimuziki.

 

Mashabiki walitakiwa kupiga kura kwa kutazama video na kisha kuandika maoni MSHINDI na pia walitakiwa ku like video husika na video iliyotazamwa mara nyingi ndiyo itaibuka kidedea na msanii kujinyakulia tuzo.

 

Akiongea wakati wa hafla fupi ya utoaji wa tuzo hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za Makampuni ya Global Group zilizopo Sinza Mori Jijini Dar, mratibu wa shindano hilo Kelvin Nyorobi alisema lengo kubwa la kuanzishwa kwa shindano hilo ni nia ya dhati ya ya Global TV Online kuwashika mkono vijana wenye vipaji lakini hawana watu wa kuwashika mkono.

“Lengo kubwa la shindano hili lilikuwa ni kuwapa sapoti wasanii chipukizi ambao hawana watu wa kuwashika mkono katika kukuza kazi zao, hivyo sisi kama Global Group kupitia Global TV tukaona tuje na fursa hii ili kuwainua vijana hawa,” amesema Nyorobi.

 

Washindi walioingia tatu bora kwenye shindano hilo ni Goweshan ambaye ameibuka mshindi kwa wimbo wake wa talent kutazamwa mara 6,356 huku ukipata likes 405.

 

Mshindi wa pili alikuwa Fetilicious ambaye video yake ya Raha ilitazamwa mara 3,329 na ikiwa na likes 145, na mshindi wa tatu alkiwa Juleizer ambaye video yake ya Kido ilitazamwa mara 2,694 na akipata likes 365.

 

Aidha, kwa upande mwingine washiriki wa shindano hilo wameupongeza uongozi wa Global Group kwa moyo wao wa kuthamini vipaji na kutoa sapoti ambayo itawafanya wao kuweza kufikia malengo yao.

 

Mshindi huyo sasa atafanyiwa promosheni kazi zake zote kwenye platforms zote za GLOBAL GROUP ambazo ni MAGAZETI, GLOBAL TV, GLOBAL RADIO, INSTAGRAM na FACEBOOK.

#LIVE: MSHINDI WA SHINDANO LA TOBOA KIMUZIKI NA GLOBAL ATANGAZWA

Leave a Comment