×

Kiwanga: Kilio cha Lijualikali ni Usanii, Kilombero Wamemchoka – Video

 

MBUNGE wa Mlimba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Suzan Kiwanga leo Jumatano, Mei 20, 2020, amefunguka kuhusu yanayoendelea ndani ya chama hicho yakiwemo masuala ya utovu wa nidhamu na tuhuma za kukisaliti chama hicho kwa baadhi ya wabunge ambao hivi karibuni wamevuliwa uanachama na kutimuliwa ndani ya chama hicho.

 

Akizungumza na Kipindi cha Front Page kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kupitia +255 Global Radio, kiwanga amesema; “Kile kilio cha Lijualikali Bungeni ni usanii tu. Kwanza alikuwa msumbufu sana, wananchi wa Kilombero wameshamchoka, na yeye ameshakata tamaa. Ameenda huko kwa sababu anajua hana nafasi tena jimboni, hatarudi tena bungeni.

 

“Kuhusu wabunge wa Chadema waliotimuliwa kabla ya kupewa nafasi ya kujitetea mimi siwezi kuzungumza sana kwa sababu sio mwenyekiti wala katibu wa chama. Huwezi kuwa mwanachama tena mbunge ukatoka hadharani na kukisema chama hovyo kwenye mitandao na vyombo vya habari na bungeni halafu ukaachwa tu, utatimuliwa mara moja. Kama hao waliotimuliwa wanaona hawajatendewa haki, basi waende mahakamani haki yao wataipata huko.

 

“Suala la mimi kukamatwa mara kwa mara kwa tuhuma mbalimbali linaniathiri sana namna ya kuwawakilisha wananchi wangu wa Mlimba. Mfano unakuwa kwenye ziara katika maeneo mbalimbali ya kata na vijiji kukagua miradi jimboni ama kuzungumza na wananchi ili kupata kero zao uziwasilishe bungeni, ghafla unapigiwa simu na RPC unaambiwa unatakiwa kituo kikuu cha polisi Morogoro, ukifika pale unaweza kuhojiwa ukaachiliwa au ukawekwa mahabusu hata wiki tatu. Inaniathiri sana. Lakini napambana kuhakikisha nawawakilisha ipasavyo wnanchi wangu,” alisema.

 

 

Leave a Comment