×

Global Habari Mei 24 -Maambukizi Ya Corona Yapungua Nchini


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Mei 24, 2020 akizungumza na waumini wa dini ya kiislam mara baada ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Fitri katika Msikiti wa Gaddafi, jijini Dodoma. Pia Rais Dkt. Magufuli amewashukuru waumini wa dini nyingine nchini kwa kushiriki kikamilifu kwenye kuliombea Taifa.

Waziri Mkuu amesema katika hospitali ya Amana yupo mgonjwa mmoja, Mloganzila yupo mmoja, Temeke hatuna mgonjwa aliyethibitishwa, Kairuki hakuna mgonjwa, Rabiansia hakuna mgonjwa, Regency hakuna mgonjwa, Aga Khan yuko mgonjwa mmoja, Lulanzi Kibaha wapo wagonjwa 16 na Dodoma Mkonze mpaka leo asubuhi wapo wagonjwa tatu.

Awali, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab, amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa kuwapa Watanzania moyo wa kishujaa na ujasiri katika kukailiana na ugonjwa wa COVID-19 kwa kuwataka wamwombe Mwenyezi Mungu ili aliepushe Taifa na janga hilo, wakati Mataifa na viongozi wengine duniani yakikumbwa na taharuki.

Leave a Comment