
Kufuatia kuwepo kwa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona nchini ambao uliripotiwa kwa mara ya kwanza mwezi Machi, mwaka huu, Serikali iliamua kusimamisha shughuli zote za michezo ikiwemo mashindano ya ligi za soka kwa lengo la kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.
Takwimu za mwenendo wa ugonjwa wa Covid-19 nchini kwa sasa zinaonesha kupungua kwa wagonjwa jambo ambalo linaleta matumaini ya kuendelea na shughuli za kijamii ikiwemo Serikali kupitia kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kuruhusu shughuli za michezo kuendelea kuanzia Juni Mosi, 2020.
Aidha, Rais aliziagiza wizara zenye dhamana ya Afya na ile ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kuandaa mwongozo wa pamoja wa namna michezo itakavyorejea nchini hususan ligi za soka.
Kwa maelekezo hayo, wataalamu na baadaye viongozi wa sekta hizi mbili, kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa michezo yakiwemo mabaraza, shirikisho, vyama na vilabu vyenyewe, wamekubaliana kuzingatiwa.
Utaratibu huu unalenga kusaidia kuwepo kwa mazingira wezeshi na salama ili kuendelea na michezo na kuepusha kuenea kwa maambukizi ya Virusi vya Corona.
Aidha, utaratibu huu utatumika ndani ya Tanzania Bara kwa michezo ya aina zote na katika ngazi zote hususan Ligi Kuu ya Soka na michezo mingine mbalimbali. Katika kufanikisha uwepo wa mazingira hayo, yafuatayo ni muhimu kuzingatiwa;-
2.0.1 Elimu kwa wadau wa michezo kuhusu kujikinga na maambukizi:
a)Wataalam wa afya kwa kushirikiana na wasimamizi wa michezo husika watoe elimu kwa wadau wa michezo kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kabla michezo yote haijaanza rasmi ikiwemo kuhusu mwongozo huu na maelekezo mengine ya wataalamu wa afya;
b)Wataalamu wa afya waendelee kusambaza mabango kwenye viwanja, vyumba vya kubadilishia nguo, kambi za michezo kwa ajili ya wachezaji na mashabiki kusoma taratibu na kanuni za kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Corona.
Aidha, mabango yawekwe pia katika maeneo yote yatakayohusisha wananchi kuangalia mashindano ya michezo;
c)Kuwepo na matangazo ya mara kwa mara ndani na nje ya viwanja vya michezo kabla, wakati na baada ya matukio ya michezo;
d)Madaktari wa timu au washauri wa afya wa vyama na mashirikisho ya michezo washiriki katika hatua hizi kikamilifu kwa kutoa semina kwa wachezaji na viongozi kuhusu mambo ya kuzingatiwa kiafya katika kila hatua za maandalizi, kambi, mechi na baada ya mechi;
e)Viongozi wengine wa vilabu, vyama, mashirikisho, timu kama vile Wenyeviti, wadhamini, wasemaji, Makatibu Wakuu, makocha na manahodha nao washiriki kikamilifu kutoa elimu na kusisitizia tatahdhari za kiafya kila wanapopata nafasi;
ENDELEA KUSOMA MUONGOZO HUO HAPA

